"UISLAM IWE SUNI AU SHIA NITISHIO KWA DUNIA MZIMA"

 

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa Uislamu  iwe wa Sunni au Shia ni tishio kwa dunia nzima, kauli ambayo imezua mjadala na ukosoaji katika duru za kimataifa.


Netanyahu alidai kuwa changamoto kubwa kwa usalama wa kimataifa inahusishwa na makundi yenye msimamo mkali yanayojihusisha na itikadi za Kiislamu, akisisitiza kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua kukabiliana na kile alichokiita hatari hiyo.


Kauli hiyo imeibua hisia tofauti, huku baadhi ya

wachambuzi wakisema inaweza kuongeza mvutano wa kidini na kisiasa katika maeneo mbalimbali duniani.