Wakazi laki 2 wilayani Musoma hatarini kiafya
Wakazi zaidi ya laki 2 katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara wanatumia maji yenye vimelea vya magonjwa ya kuambukiza,jambo linalofanya kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza mara kwa mara. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Dkt. Khalfan Haule wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu,kutokana na wananchi kutumia maji ya ziwa Viktoria. Kwa mujibu wa sampuli 14 zilizopimwa za maji wanayotumia wakazi hao zilionekana maji hayo kuchanganyika na kinyesi cha binadamu jambo linalochochea ugonjwa wa kipindupindu kushamiri eneo hilo. Mkurugenzi huyo amesema kati ya wagonjwa 10 wanaougua kipindupindu 7 ni wavuvi jambo linaloashiria ukweli wa sampuli zilizopimwa ambapo tangu ugonjwa huo umeingia watu 789 wameambukizwa na 37 kupoteza maisha. Aidha Mkuu wa wilaya ya Musoma ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Zelote Steven amesema ni wakati wa kuacha siasa kwa watendaji kuelekea maeneo hus...