Idadi Ya Watumishi Hewa Iringa Yaongezeka Nje Ya Ile Aliyopewa Rais Magufuli
Hadi kufikia tarehe 18/04/2016 Mkoa wa Iringa umefanya zoezi la uhakiki wa watumishi kwa awamu mbili awamu ya kwanza, uhakiki ulifanyika kuanzia tarehe 16/03/2016 na kukamilika tarehe 26/03/2016 ambapo jumla ya watumishi 15walibainika kuwa ni watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa ambao waliisababishia Serikali hasara ya Shilingi 81,921,725.08. Katika uhakiki wa awali Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo haikuwahakiki watumishi 159 kutokana na kuwa masomoni. Halmashauri hiyo imekamilisha uhakiki huo ambapo imebainika watumishi wawili (2) ni watumishi hewa. Ndugu Waandishi wa Habari, Ili kuhakikisha Mkoa unaondokana kabisa na tatizo la watumishi hewa, niliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya zoezi hilo awamu ya pili. Nimepokea taarifa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya inayoonesha kuwapo kwa watumishi hewa kumi na mbili (12) hadi kufikia tarehe 18/04/2016. Watumishi hao wameisababishia Serikali hasara ya shilingi ...