SIMBA INAJIFUNGA YENYEWE
Unaweza kusema Simba ni kama imejifunga yenyewe kwenye mchezo wake wa ligi wa Jumapili dhidi ya Toto Africans ya Mwanza au kwa maneno ya vijana wa mjini wanasema ‘wamejilipua’ wenyewe kwa mabomu yao. Katika kikosi cha Toto Africans kilichoichapa Simba 1-0, kiliundwa na wachezaji vijana wa walionunuliwa na Toto kutoka Simba. Wachezaji hao ni Carlos, Chuku, Hassan Hatib ambao wote walicheza kwenye aneo la ulinzi, Seseme alicheza kama kiungo wa kati wakati Edward Christopher alicheza kama mshambuliaji. Kwenye benchi alikuwepo Japhet wakati wachezaji wengine ambao hawakuwepo kwenye plan ya mechi hiyo ni Miraji Madenge na Ahmad Waziri ‘Kuku’. Ilikuwa ni lazima Simba wafungwe kutokana na kocha wa wa Toto John Tegete kuwaamini vijana watano aliowachukuwa kutoka Msimbazi na kuwaambia kuwapa majukumu ya kudhihirisha kwamba, wao ni bora na walistahili kukitumikia kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na uwezo mkubwa waliokuwa nao. Klabu ya Simba imepoteza hazina...