Watumishi HEWA Wakopa Mamilioni ya Pesa Benki......TAMISEMI Mwanza Yaongoza kwa Rushwa
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale ******* TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imebaini kuwepo kwa watumishi hewa zaidi ya watano ambao uongozi wa mkoa huo haukuyawasilisha majina yao kwa Rais Dk. John Magufuli huku yakionekana kukopa fedha benki. Pia Takukuru imesema kuwa majina ya watumishi hewa hao baada ya kufanya uchunguzi wamebaini hukopeshwa fedha kwa kisingizio kwamba wao ni watumishi wa Serikali kitendo ambacho ni cha uongo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale wakati akitoa taarifa ya robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, ambako alisema majina yaliowasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella sio kamilifu. Amesema watumishi hao hewa wamekuwa wakikopa fedha kutoka benki mbalimbali kwa kutumia nyaraka za kughushi jambo ambalo alidai kwamba kuna baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaohusika kufanya udanganyifu huo. Amesema pia katika uch...