Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya AZAM FC ‘WANASHANGAZA’ SANA KATIKA MACHAGUO YAO YA MAKOCHA

AZAM FC ‘WANASHANGAZA’ SANA KATIKA MACHAGUO YAO YA MAKOCHA

Picha
AZAM FC  wanashangaza sana kwa kweli! Ukiniuliza Azam inahitaji nini zaidi? Jibu langu ni kocha bora mwenye uzoefu na mpira wa Afrika. Mfano, Mnigeria, Stephen Keshi ama pengine Mscotland, Bobby Williamson ambaye kwa miaka nane amekuwa na kazi yenye mafanikio katika Afrika Mashariki na Kati. Sijui lolote kuhusu kocha Mspaniola ambaye ameingia nchini Ijumaa kufanya mazungumzo ya kukinoa kikosi hicho ambacho kwa hakika kitashiriki katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baadae mwaka ujao. Nilikwisha andika mara kadhaa kuhusu uwezo wa kiufundishaji wa kocha wa sasa Muingereza, Stewart Hall ambaye kwa mara ya tatu ndani ya miaka minne ataachia kazi. Azam FC imejipotezea muda kwa uamuzi wake wa kumrejesha Hall ili kuchukua nafasi ya Mhindi, Boris Bunjak mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2012/13. Hall alijiunga kwa mara ya kwanza na Azam FC mwezi Disemba  2010 akitokea Zanzibar alikokuwa akiinoa timu ya Taifa ‘Zanzibar Heroes....