Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Majambazi Yaliyotoroka Mapangoni Jijini Mwanza Yazua Hofu......Baadhi ya Wananchi Waanza Kuyahama Makazi Yao

Majambazi Yaliyotoroka Mapangoni Jijini Mwanza Yazua Hofu......Baadhi ya Wananchi Waanza Kuyahama Makazi Yao

Picha
Siku moja baada ya kutokea mapambano ya zaidi ya saa 16 baina ya Jeshi la Polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwenye mapango ya mlima ya Utemini, wananchi wa eneo hilo wameingiwa na hofu ya usalama wao baada ya baadhi yao kuona wahalifu wakitoroka wakati wa tukio hilo. Wananchi hao wana hofu kuwa majambazi waliotoroka wanaweza kurejea na kuwadhuru na tayari baadhi wameanza kuhama makazi yao. Hofu ya wananchi hao imekuja baada ya polisi kupambana na watu hao usiku wa kuamkia juzi, wakitumia silaha kali zilizo sababisha kizaazaa kwa wakazi wa Utemini, kutokana na milio ya risasi na mabomu. Mwenyekiti wa Mtaa wa Utemini Ibanda, kata ya Mkolani, Jukael Kiula jana alisema baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na mapango hayo wameanza kuhama makazi yao wakihofia kurejea kwa majambazi hao. “Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya majirani, walikuwa wakiwaona watu wakipanda na kushuka kutoka kwenye milima yenye mapango waliyojificha watu hao. Lakini hawakuwatilia shaka...