Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wasaliti Ndani ya CCM Waanza Kutumbuliwa MAJIPU

Wasaliti Ndani ya CCM Waanza Kutumbuliwa MAJIPU

Picha
Huku kukiwa na taarifa kuwa wasaliti wa CCM wanaotarajiwa kutimuliwa wengi ni watu maarufu hasa viongozi wa ngazi za mkoa, tayari viongozi 21 wa Manyara, wameshatumbuliwa majipu bila ganzi. Jumla ya viongozi 21, watatu wakiwa ni wa CCM Wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara na wengine 18 wa ngazi ya kata, wameshaadhibiwa na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alichokiita kutumbua majipu bila aibu. Inadaiwa kuwa viongozi hao walikuwa wanamshabikia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa. Imedaiwa ushabiki ulisababisha CCM ipoteze jimbo na kata tano kati ya nane za Babati Mjini. Katibu wa CCM mkoani Manyara, Ndeng’aso Ndekubali aliwataja waliofukuzwa uanachama kuwa ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Cosmas Masauda, Zulekha Mohamed na mjumbe wa mkoa, Felix Kivuyo. “Hawa wamefutwa uanachama baada ya kudaiwa kukisaliti chama kwa kuwapigia kampeni wagombea wa vyama vya upinzani na kuwaombea kura kwenye Uchaguzi Mkuu,” alidai Ndekubali. Februari 24, mwaka...