Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais Magufuli Atoa Mchango wa Milioni 10 Kusaidia Matibabu ya Mwafunzi Aliyepata Upofu

Rais Magufuli Atoa Mchango wa Milioni 10 Kusaidia Matibabu ya Mwafunzi Aliyepata Upofu

Picha
Rais John Magufuli ametoa mchango wa Sh. milioni 10 kwa ajili kusaidia matibabu ya mwanafunzi Bernadetha Msigwa aliyepata upofu hivi karibuni. Msichana huyo anayesoma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, ni miongoni wa wasichana ambao tatizo lake limeibuliwa kupitia kampeni ya Kipepeo, iliyoanzishwa na kampuni ya Clouds Media, Mei Mosi mwaka huu. Kupitia matangazo yanayorushwa na kampuni hiyo, Rais Magufuli baada ya kusikia tatizo la Msigwa, ambaye pia picha yake imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, akiwaomba Watanzania wamsaidie mchango wa fedha ili aweze kutibiwa. aliguswa na kuamua kutoa mchango huo. Meneja wa kipindi cha 360 kinachorushwa kila siku za wiki asubuhi na televisheni ya Clouds, Hudson Kamoga alisema baada ya Rais kuona tangazo hilo, lililorushwa muda mfupi kabla ya kuanza uchambuzi wa magazeti, alimpigia simu. “… Alisema ameguswa na stori ya Bernadetha, hivyo yeye na familia yake watachangia Sh10 milioni ili kumsadia,” alisema Kamo...