Steven Wasira Amkunja Shati Mwandishi Baada Ya Kesi Yake Kupinga Ushindi wa Ester Bulaya Kutupiliwa Mbali Na Mahakama
Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani, lakini akashindwa kutimiza azima yake ya kufuta picha. Wasira, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wa Serikali ya Awamu ya Nne (SA4), alifanya kitendo hicho akitoka kwenye jengo la Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupwa na Mahakama Kuu. Katika kinyang’anyiro hicho cha ubunge, Wasira, ambaye amekuwa mbunge wa Mwibara tangu mwaka 1970 na baadaye mbunge wa Bunda hadi mwaka 2015, aliangushwa na Ester Bulaya wa Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana. Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari akiwamo walishuhudia tukio hilo. “Wasira alimkimbiza Jamson akitaka kumnyang’anya kamera, lakini hakuweza,” alisema Nyange,mwandishi wa gazeti la Mtanzania. “Baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati...