Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Yamuonya Uhuru Kenyatta
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetishia kuichukulia Kenya hatua kali isiposalimisha kwa mahakama hiyo washukiwa watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya kutatiza mashahidi. Msemaji wa ICC Fadi el Abdallah alisema mahakama hiyo itairipoti Kenya kwa Baraza la Mataifa Wanachama wa Mkataba wa Roma (ASP) kama itaendelea kushikilia msimamo wa kutowawasilisha Wakenya hao watatu mbele ya mahakama hiyo mjini Hague, Uholanzi. Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Bi Fatou Bensouda, amepata kibali cha kuwakamata aliyekuwa mwanahabari Walter Osapiri Barasa, wakili Paul Gicheru na Philip Bett kwa madai ya kutatiza mashahidi katika kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang. Agizo la kukamatwa kwa Bw Barasa lilitolewa Oktoba 2013 ilhali lile la kukamatwa kwa Philip Bett na Paul Gicheru lilitolewa Septemba 2015 kwa madai kuwa walihonga mashahidi. Kesi dhidi ya Bw Ruto na Sang ilitupiliwa mbali mapema mwezi huu kwa misingi kuwa ilikosa ushahidi wa kutosha kuto...