Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Takukuru Yalia na Rushwa Mahakama ya Kisutu

Takukuru Yalia na Rushwa Mahakama ya Kisutu

Picha
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameiomba mahakama iingilie kati kile alichokiita rushwa ya kutisha kwenye taasisi hiyo ya kutoa haki. Wakili Swai alitoa wito huo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu kumuachia huru mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Geofrey Mhando na wenzake wanne akiwamo mkewe Eva Mhando, katika kesi aliyokuwa akiiendesha.  Katika kesi hiyo, Mhando, mkewe na maofisa wengine watatu wa zamani wa Tanesco; France Lucas Mchalange, Sophia Athanas Misida na Naftali Luhwano Kisinga, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali. Hata hivyo, washtakiwa hao wameibwaga Takukuru baada ya mahakama kuona kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao. “Haki haijatendeka na tunatarajia kukata rufaa,”  alisema Wakili Swai alipozungumza na waandishi nje ya mahakama. ...