Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sasa Kusajiliwa Kwa Kuchukuliwa Alama za Vidole 10.........Wapiga Picha za Tv na Redio Marufuku Bungeni

Wabunge Wabanwa, Sasa Kusajiliwa Kwa Kuchukuliwa Alama za Vidole 10.........Wapiga Picha za Tv na Redio Marufuku Bungeni

Picha
Bunge  linaanza rasmi usajili wa wabunge na watumishi wa Bunge hilo pamoja na wageni mbalimbali, wanaoingia bungeni kwa kutumia mfumo wa kisasa wa kuchukua alama za vidole. Sambamba na mfumo huo, Bunge pia limetoa taarifa rasmi ya kudhibiti urushaji wa matangazo ya Bunge ambayo sasa vyombo vya habari vya kielektroniki havitaruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa bunge na kamera kwa lengo la kurekodi yanayoendelea. Na badala yake, jukumu la kurusha matangazo ya vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia Feed Maalum ili kurahisisha kila kituo cha redio na televisheni kupata matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga mitambo yao bungeni. Hayo yalibainishwa jana na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah wakati akitoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge hilo, Dk Tulia Ackson alipofanya ukaguzi wa ukarabati uliofanywa ndani ya Ukumbi wa Bunge linaloanza vikao vyake vya Bajeti katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11 mjini hapa. Dk Kashilillah alisema kuanzia jana wabunge wataanz...