Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waziri Nchemba Awapasha Wafugaji na Wakulima

Waziri Nchemba Awapasha Wafugaji na Wakulima

Picha
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, amewataka wakulima na wafugaji kuacha kutumia uhai wa mtu kama fidia ya mifugo au mashamba yaliyoharibiwa kwa kuuana katika mapigano ya wenyewe kwa mwenyewe. Nchemba alisema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza jipya la wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.    Alisema vitendo vya mauaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na jamii za wafugaji na wakulima kuuana havistahili kuendelea kuwapo katika jamii iliyostaarabika.    Mwigulu alisema hakuna mifugo wala mashamba yenye thamani zaidi ya maisha ya binadamu, hivyo jamii hizo mbili zinatakiwa kutafuta namna sahihi ya kutatua migogoro baina yao na siyo kuendeleza mapigano na kupoteza maisha ya binadamu wenzao.    “Ni aibu sana mtu kuua kwa ajili ya shamba au mifugo kwakuwa hakuna kitu kinachoweza kulinganishwa na maisha ya mtu, hivyo basi fidia za mifugo au shamba zifanyike kwa vitu na siyo maisha y...