CCM YAWASHUKIA WAPINZANI KUHUSU KUGOMEA GOMEA KWAO BUNGE LIVE
"Wakati watu wanakwepa kodi bandarini, hakuna mbunge wa upinzani aliyetoka Bungeni kwenda kwa wananchi kulalamikia utendaji wa Serikali; "Wakati wa ukwepaji mkubwa wa kodi kutokana na uagizwaji wa sukari, hakuna mbunge wa upinzani aliyetoka Bungeni kwenda kwa wananchi kulalamikia utendaji wa Serikali; "Leo Rais Dkt. John Magufuli anawabana wakwepa kodi na kuirudisha nchi kwenye mstari, wabunge wa upinzani wanatoka Bungeni na kudai kuwa wanakwenda kumshtaki Rais kwa wananchi kuwa anaendesha nchi kidikteta! "Ni wazi hawa watu hawajitambui na wala hawatambui wajibu wao wa uwakilishi wa wananchi." Christopher Ole-Sendeka Msemaji wa CCM