Rais Magufuli Aungana Na Rais Kenyatta wa Kenya Kuomboleza Kifo Cha Mke wa Rais Mstaafu Mama Lucy Kibaki
Marehemu Lucy Kibaki akiwa na Mumewe Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Mwai Kibaki siku ya ndoa yao mwaka 1962. ******** Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya mheshimiwa Uhuru Kenyatta,kufuatia kifo cha mke wa Rais Mstaafu wa Kenya mama Lucy Kibaki aliyefariki dunia leo tarehe 26 April 2016 Mama Lucy Kibaki ambaye ni mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki amefariki dunia jijini London nchini uingereza ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Katika salamu hizo,Rais Magufuli ameeleza kushtushwa na kifo hicho na kuongeza kuwa Kenya imempoteza mtu mhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yake. "Kupitia kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole nyingi Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki,Familia yake,ndugu,jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa." Amesema Rais Magufuli. Dkt John P...