IJUE SAGRADA ESPERANCA ‘MWADUI YA ANGOLA’ AMBAYO ITECHEZA NA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO
Na Athumani Adam Esperanca kwa sasa wanafundishwa na kocha kutoka Serbia, Zoran Mackic.Wana wachezaji watano raia wa kigeni, wareno wawili, wakongo wawili na mghana mmoja.Timu hii inatoka mji wa Dundo, mji wenye utajiri wa madini ya dhahabu na almasi. Grupo Desportivo Sagrada Esperanca kutoka Angola wamefikia tena rekodi yao kwenye michuano ya ngazi ya vilabu barani Afrika. Mara ya mwisho kuweka rekodi yao ya juu kwenye michuano hii ilikua mwaka 2005 pale walipotolewa na Asec Abidjan ya Ivory Coast kwa jumla ya magoli 3-2 raundi ya 16 bora klabu bingwa barani Afrika. Mwaka huu watacheza na Yanga ya Tanzania kwenye raundi ileile ya 16 bora lakini siyo klabu bingwa Afrika bali ni kombe la shirikisho. Esperanca wamefanikiwa kukutana na Yanga baada ya kutolewa na Vita Klabu ya Jamuhuri ya Kongo ambapo Yanga walitupwa nje na Al Alhy ya Misri kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika. Kuelekea mchezo wa kwanza kati yao ambao utachezwa kati ya Mei 6 hadi 8 jijini D...