LEO KATIKA HISTORIA: MATUKIO MANNE YALIYOJIRI JUNE 7 ENZI HIZO
Picha hii ni ya mwaka 1973-Yanga ilicheza na Aston Villa mabingwa wa Ulaya mwaka 1981-1982 kutoka England. Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao na Aston Villa wakasawazisha dakika za lala salama Kuna matukio mengi sana yakukumbukwa kila siku kwenye ulimwengu wa michezo na hii nikutokna na rekodi na matukio mbalimbali yaliyopita siku za nyuma na kugeuka historia. Kwa upande wa soka, leo June 7, 2016 kuna matukio kadhaa makubwa ya kukumbukwa ambayo yalitokea siku kama ya leo miaka mingi iliyopita na kuacha alama kwenye medani ya soka la Bongo. shaffihdauda.co.tz inakusogeza karibu na matukio manne ya kukumbukwa kwenye anga la soka hapa nchini ambayo yalijiri tarehe na mwezi kama wa leo katika miaka minne tofauti. 1965: Yanga ya Dar es Salaam yaifunga Sunderland nayo ya D’Salaam (1-0) 1989: Waziri Charles Kisanji auvunja uongozi wa chama cha soka nchini-FAT 1998: Simba na Yanga zatoka sare (1-1) 2007: Timu ya soka ya Azam FC inaundwa 2014: Ali Hassan Mwanakatwe, Katibu Mkuu ...