Kiwanda Bubu Cha Kutengeneza Pafyumu Feki Chakamatwa Dar es Salaam
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamekamata kiwanda bubu kinachotengeneza pafyumu bandia kilichopo eneo Tuangoma, mtaa wa Goroka Wilala ya Temeke. Kukamatwa kwa kiwanda hicho kinachotengeneza pafyumu aina ya SAME, kunatokana na TFDA kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna shehena kubwa ya pafumu hizo katika duka moja la vipodozi lililopo Sinza kwa Remmy wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hiiti Sillo alisema TFDA kanda ya mashariki baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa kiwanda hicho kutoka kwa wasamaria wema, walifanya ukaguzi katika duka hilo la vipodozi na kukamata chupa 5,350 za pafyumu aina ya SAME zenye thamani ya Sh 107 milioni. “Februari 23,mwaka huu tulifanya ukaguzi katika duka hilo lililopo Sinza kwa Remmy na kukuta pafyumu 5,350 ambazo zinauzwa Sh 20,000 kwa chupa moja ya pafyumu na pia tuligundua kuwa duka na pafyumu hizo zilikuwa ha...