Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Paul Makonda Asema Baadhi ya Ombaomba Wanauza Madawa ya Kulevya

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda Asema Baadhi ya Ombaomba Wanauza Madawa ya Kulevya

Picha
Mkuu  wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, ombaomba walioko jijini Dar es Salaam baadhi yao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya. Akihojiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha redio, Makonda alisema wapo watu ambao wanatumia mwanya huo kusambaza dawa za kulevya. “Wapo wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,”  alisema Makonda. Makonda aliwataka wakazi wa jiji hilo kushirikiana naye katika kuwaondoa ombaomba hao ambao wengi wanatoka nje ya Da es Salaam na kwamba hakuna tija kuendelea kuwaacha.  “Watanzania tuna upendo sana lakini tunahitaji kutafakari kama kweli watu walioko barabarani wakiomba kama kweli wanahitaji msaada huo au la,”  alisema Makonda. Alisema kwa kuendelea kuwaacha ombaomba hao pia kutasababisha vijana ambao sasa wanao...