ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI ,AKANA SHITAKA
ARUSHA MKAZI wa Olasiti Jijini Arusha, Isaac Emily (40), amepandishwa kizimbani kwa kumtolea maneno ya dharau na kumdhihaki Rais John Magufuli katika mitandao ya kijamii. Alisomewa mashitaka jana na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Gaudencia Masanja mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile. Mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais, Isaac Emire (katikati) akiongozwa na askari kuelekea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu mashtaka ya kesi hiyo jana. Katika mashitaka hayo, Emily amedaiwa kutenda kosa hilo Machi 17 mwaka huu kinyume na sheria ya mitandao namba 16 kifungu namba 14 ya mwaka 2014. Masanja alidai kuwa, siku hiyo mshitakiwa alisambaza ujumbe wa uongo katika mitandao ya kijamii wenye lengo la kumdharau, kumdhihaki na kumtolea maneno Rais Magufuli yenye lengo la kumdhalilisha. Alidai kuwa ujumbe huo ulisomeka, ”Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi bwana.’’ Mshitakiwa huyo alikana kutenda...