Majaliwa Akutana Na Wawekezaji Wa Umeme Wa Gesi Toka Japan
Shirika la Koyo la kutoka Japan limepania kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na umeme jua ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi waishio vijijini. Hayo yamesemwa jana jioni (Jumatatu, Mei 9, 2016) na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa shirika la Koyo, Bw. Norio Shoji wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. “Tumepanga kuwekeza kwenye maeneo matano ambayo mojawapo ni kujenga mtambo wa kuchakata gesi kwa kutumia gesi asilia inayozalishwa hapa nchini. Mtambo huu utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1,000 za umeme,” alisema. “Pia tunao mpango wa kujenga mitambo ya umemejua inayoweza kujiunganisha kwenye gridi (on-grid/off grid solar power plants) kwa ajili ya maeneo vijijini na yale yasiyofikika kwa urahisi zaidi ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa usambazaji umeme kwenye gridi ya Taifa ili Tanzania iweze kuzalisha zaidi nishati hiyo na kuiuza nchi jirani,” aliongeza. Bw. Sh...