Hali tete ya Libya
Hali ya mambo nchini Libya inatajwa kuwa ni tete licha ya kuanza kazi serikali ya umoja wa kitaifa iliyoungwa mkono na kukaribishwa na jamii ya kimataifa. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya, Martin Kobler ametangaza kuwa wafanyakazi wa ofisi ya umoja huo wamerejea Libya kwa ajili ya kuanza shughuli zao. Kobler amesema maafisa hao wanahitajia mawasiliano ya kudumu na pande zote za kisiasa na makundi ya jamii ya Libya. Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliondoka Libya katika vita vya msimu wa joto wa mwaka 2014 baada ya muungano wa makundi yenye silaha unaojiita Fajr Libya kudhibiti mji wa Tripoli. Wakati huo huo Naibu Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ametangaza kuwa, Wizara za Michezo na Vijana, Masuala ya Jamii, Nyumba na ya Huduma za Umma zitakabidhiwa kwa serikali ya maridhiano ya kitaifa hii leo Jumatatu. Libya ambayo ilitumbukia katika machafuko na ghasia baada ya kuondolewa madarakani utawala wa Kanali Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011, ka...