Utata ACT – Wazalendo..Zitto Kabwe Adaiwa Kumpindua Mwigamba ili Achukue Nafasi yake
Mwigamba, Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameng’atuka rasmi nafasi hiyo kwa madai kuwa anaenda masomoni, anaandika Pendo Omary. Anna Mghwira, Mwenyekiti wa chama hicho ameliambia MwanaHALISI Online kuwa, Samson Mwigamba ataanza masomo ya shahada ya Uzamili ya Biashara (MBA) katika Chuo Kikuu cha Kenyata tawi la Arusha kuanzia mwezi Mei mwaka huu. “Kufuatia hatua hii ameomba aruhusiwe kung’atuka nafasi yake ya Katibu Mkuu wa chama. Katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana katika Hotel ya Kebby’s Jijini Dar es Salaam, Kamati ya Uongozi Taifa imeridhia ombi la Katibu Mkuu,” amesema Mghwira. Mghwira amesema kufuatia hatua ya kung’atuka kwa Mwigamba, Kamati ya Uongozi ya chama hicho imeiagiza kamati ya Mafunzo na Uchaguzi ianze mchakato wa kumpata katibu mkuu mpya kwa kuzingatia katiba na kanuni za uchaguzi wa chama. Aidha, Mwigamba amesema hatua hiyo haimzuii kushiriki katika shughuli zingine za chama atakap...