Hizi Hapa Ndio Dawa za Hospitalini Zinazopunguza Ama Kuua Nguvu za Kiume Kwa Wanaume
Dawa zote zinazopatikana mahospitalini na maduka ya madawa zinaletwa kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali, japokua baadhi ya dawa hizo huambatana na madhara madogo na makubwa kwenye mwili wa binadamu. madhara madogo madogo huweza kua kichefuchefu,kizunguzungu, kutapika, kuharisha na kadhalika. na madhara makubwa huweza kua kansa, madonda ya tumbo, ugumba, kuishiwa nguvu za kiume na kadhalika. leo ntaenda kuongelea dawa za hospitalini ambazo zinhusika sana kuua nguvu za kiume na kama una tatizo hili uziepuke mara moja. Dawa za kutibu presha; kuna dawa nyingi sana za kutibu presha na hufanya kazi kwa njia tofauti tofauti yaani ikishindwa hii unapewa nyingine na zifuatazo ni baadhi ambazo huua nguvu za kiume. mfano Hydrochlorothiazide, Hydropres, Inderide, Moduretic, Oretic, Lotensin, Chlorthalidone (Hygroton), Triamterene (Maxide, Dyazide), Furosemide (Lasix), Bumetanide (Bumex), Guanfacine (Tenex), Methyldopa (Aldomet), Clonidine (Catapres), Verapamil (Calan, Isoptin, V...