Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo tarehe 25 April 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo tarehe 25 April 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa. Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo; ⦁ Arusha – Richard Kwitega ⦁ Geita – Selestine Muhochi Gesimba ⦁ Kagera – Armatus C. Msole ⦁ Kilimanjaro – Eng. Aisha Amour ⦁ Pwani – Zuberi Mhina Samataba ⦁ Shinyanga – Albert Gabriel Msovela ⦁ Singida – Dr. Angelina Mageni Lutambi ⦁ Simiyu – Jumanne Abdallah Sagini ⦁ Tabora – Dkt. Thea Medard Ntara ⦁ Tanga – Eng. Zena Said Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo; ⦁ Kigoma – Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita) ⦁ Morogoro – Dkt. John ...