Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya JOSEPH

WAZAZI WALALAMIKA KUFUNGWA KWA MATAWI YA CHUO KIKUU CHA ST, JOSEPH

Picha
BAADHI   ya wazazi wa wanafaunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika  matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao. February 26 mwaka huu ,tume ya vyuo vikuu ilitangaza kufuta kibali cha chuo kikuu cha St Joseph (SJUIT) tawi la Arusha ikiwa ni wiki moja imepita tangu kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo kwa Chuo kikuu cha St Joseph tawi la Songea,vyuo vilivyoko chini ya shirika la kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI). Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na hatua hiyo huku wakidai kuwaathili kisaikolijia watoto wao ambao wengine walikuwa katika maandalizi ya mitihani. “Nadhani ingekuwa ni jambo la busara  kwa TCU kukaa meza ya mazungumzo na uongozi wa chuo badala ya kuchukua hatua ya kukifutia vibali….Chuo hiki kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kuzalisha wa...