Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Katibu Mkuu wa CHADEMA

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji Amemtaka Rais Magufuli Apunguze Utumbuaji Majipu

Picha
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa Serikali  Alisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi. “Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji. “Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.  Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake. “Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani laki...