Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Washtakiwa wa Tumbili 61 Wanyimwa Dhamana

Washtakiwa wa Tumbili 61 Wanyimwa Dhamana

Picha
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi imetupilia mbali maombi ya dhamana ya washtakiwa saba wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Wanyamapori Matumizi Endelevu, Dk Charles Mulokozi na wenzake sita, wakiwamo raia wawili wa Uholanzi. Dk Mulokozi na wenzake walikamatwa Machi 23, mwaka huu wakitaka kusafirisha tumbili wekundu 61 kwenda nchini Armenia. Wanyama hao walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).  Akitoa uamuzi huo juzi, Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Aishiel Sumari ambaye anasikiliza shauri hilo namba 1/2016, alisema mahakama hiyo imepima kwa umakini maombi ya dhamana dhidi ya washtakiwa hao na imeona hayana msingi, kwa kuwa suala lililopo mahakamani linagusa masilahi mapana ya Taifa.  Jaji Sumari alifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza maombi ya dhamana yaliyofunguliwa na mawakili wa utetezi, Majura Magafu, John Masangwa, Robert Rogath, Elibariki Maeda na Edward Silvester wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakilis...