Ripoti ya CAG Yaanika 'Madudu' Kibao Serikalini
Wakati Rais John Magufuli akipambana dhidi ya ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi na uovu mwingine dhidi ya mali za umma, ripoti mpya ya ukaguzi iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha ana kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita hiyo. Ripoti hiyo ya mwaka 2014/ 2015 iliyowasilishwa bungeni jana na CAG Mussa Juma Assad imeibua uozo zaidi kwenye halmashauri, taasisi za Serikali na mashirika ya umma, ikibainisha kuwa nchi ina tatizo kubwa zaidi ya watu ambao wamekuwa wakishughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano. Ripoti hiyo ya pili ya Professa Assad tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo mwaka juzi, imegusa taasisi zilizowahi kuwa chini ya Rais John Magufuli na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi Asha Rose Migiro, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba. Ripoti hiyo pia inaonyesha ufisadi katika ununuzi na uingiaji mikataba uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), matumizi yas...