Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAMA SNURA AANGUKA GHAFLA

MAMA SNURA AANGUKA GHAFLA,NI BAADA YA CHURA KUFUNGIWA

Picha
  Wakati Wabongo wakiwa wamecharuka mitandaoni kuuzungumzia wimbo wa Chura wa Snura Mushi, nyuma ya mijadala hiyo, kuna habari ya kuhuzunisha, mama mzazi wa msanii huyo, Doto Sanzegara, alijikuta akianguka kwa mshtuko baada ya serikali kutangaza kumzuia mwanaye huyo kujihusisha na kazi za sanaa, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi.  ALIZUIWA NA BASATA  Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) walitoa tamko la wimbo huo kutopigwa katika vituo vya redio na televisheni nchini pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kwa kile walichoeleza kuwa umekiuka maadili hivyo pia kumfungia kazi zake mpaka pale atakapojisajili katika chombo hicho kwa kuwa licha ya kufanya kazi za sanaa kwa muda mrefu, msanii huyo hakuwa amejisajili.  HABARI KAMILI  Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia, wakati serikali inatoa tamko la kumsimamisha Snura, Mei 4, mwaka huu, mama huyo alipata taarifa kupitia redio, ndipo alipopata mshtuko, akaanguka na kupoteza fahamu. “Yaa...