Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkutano wa kiusalama wafanyika katika msikiti mmoja nchini Rwanda

Mkutano wa kiusalama wafanyika katika msikiti mmoja nchini Rwanda

Picha
Wakuu wa vyombo vya usalama na viongozi wa Kiislamu wa Rwanda wamefanya mkutano katika msikiti mmoja nchini humo kujadili mustakabali wa kiusalama. Viongozi wa Kiislamu waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika msikiti mmoja wa wilaya ya Ruhango wameelezea juu ya utayarifu wao wa kushirikiana na vyombo vya usalama nchini humo, kwa lengo la kuboresha usalama wa eneo hilo na nchi nzima kwa ujumla. Sheikh Ismail Ntawukuriryayo, Imamu wa Msikiti wa Ruhango amesema jamii ya Waislamu nchini humo inathamini usalama na amani ya nchi na kwamba daima imekuwa ikionyesha utayarifu wake wa kuzidi kushirikiana na vyombo vya usalama juu ya suala hilo. Ameongeza kuwa, na hapa tunamnukuu: "Yale yote tuliyojifunza kwenye mkutano huu wa pamoja na vyombo vya usalama, tutayapeleka katika misikiti mingine kote nchini ili kuhakikisha kuwa jamii ya Waislamu wa Rwanda inafahamu kuwa jukumu la usalama sio tu la vyombo vya usalama, bali linahusu kila mmoja." Mwisho wa kunukuu. Kwa upande wake, ...