TCU yafuta Chuo Kikuu kingine
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imekifutia kibali cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania (SJUIT), kampasi ya Arusha kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya migogoro kati ya uongozi na wanafunzi. Februari 19, mwaka huu TCU ilivifuta vyuo vikuu vishiriki vya SJUIT kutokana na kukiuka sheria na utaratibu wa uendeshaji. Migogoro hiyo kati uongozi na wanafunzi imekuwa ikijitokeza mara kwa marakwa sababu ya matatizo ya ubora, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu kama zilivyoainishwa na TCU. Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya alisema jana kwa kipindi kirefu tume hiyo imekuwa ikifuatilia kwa karibu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki, ikiwamo kutoa maelekezo kwa uongozi wa chuo hicho kurekebisha kasoro zinazosababisha migogoro. “Licha ya jitihada za TCU kuomba uongozi wa chuo hiki kurekebisha kasoro ili kitoe elimu inayokidhi viwango, lakini hawakuzingatia. “Kama mtu hafuati utaratibu wa sheria, anapewa vigezo halafu y...