Ofisi ya Bunge Yalivaa Gazeti la Nipashe....Yalitaka Liombe Radhi
Ofisi ya Bunge imebaini upotoshwaji mkubwa Katika habari iliyochapishwa na Gazeti la Nipashe toleo la Aprili 16, 2016 yenye kichwa cha habari kisemacho “ Bunge sasa laufyata mkataba wa Lugumi”. Habari hiyo imeandikwa kufuatia ufafanuzi uliotolewa na Bunge jana kuhusu maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) dhidi ya utekelezaji wa mkataba wa Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa utambuzi wa alama za vidole (AFIS) (Automated Fingerprint Identification System.) Ndani ya habari hiyo pia, Gazeti hilo limeeleza kuwa kamati ya PAC iliwahi kuliandikia Jeshi la Polisi kulitaka liwasilishe mkataba huo mbele ya Kamati, jambo ambalo si kweli bali ni upotoshwaji wa makusudi wenye lengo la kujenga hisia mbaya kuhusu mwenendo wa shughuli za Bunge mbele ya Umma. Ukweli ni kwamba PAC haijawahi kuliandikia jeshi la Polisi kama inavyodaiwa na Gazeti hilo. Nukuu ya maelezo ya PAC katika Hansard kwa Af...