Madiwani wa UKAWA Wavamia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji La Dar Wakitaka Kuelezwa ni Lini Uchaguzi wa Meya Utafanyika
Zaidi ya madiwani 20 wanaotokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana walivamia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kumshinikiza Kaimu Mkurugenzi wake, Sarah Yohana kuitisha Baraza la madiwani kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa meya na naibu wake. Madiwani hao waliovamia ofisi hiyo jana, walisema kikao hicho kinatakiwa kuitishwa ndani ya siku saba kikiwa na ajenda moja ambayo ni uchaguzi wa meya na naibu wake, ambao umekwama mara kadhaa kwa kile walichodai kuwa ni hila na hujuma. Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, Januari 23 uliahirishwa kutokana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene kutoa muda kwa mameya wa manispaa zinazounda Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; Kinondoni, Temeke na Ilala kuandaa mfumo bora wa kuwapata wajumbe watatu watakaounda Baraza la Jiji. Februari 8, uliahirishwa kutokana na kubainika kwa nyongeza ya majina 14 yaliyopenyezwa kutoka halmashauri za Kinondoni na Ilala ambao h...