Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CHADEMA Kuishitaki Serikali Kwa Wananchi

CHADEMA Kuishitaki Serikali Kwa Wananchi

Picha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuanza ziara ya kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusiana na utumbuaji majipu usiofuata maadili ya kazi na kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya vikao vya Bunge. Mratibu wa ziara hiyo, Singo Benson alisema ziara itaanza Juni 7 katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuendelea mikoa mingine, lengo ni kuelimisha wananchi juu ya ubakwaji wa demokrasia. “Wananchi wananyimwa haki ya msingi ya kutoona matangazo ya Bunge moja kwa moja na hakuna sababu ya msingi iliyotolewa, hivyo lazima tuwaelimishe na tuwatetee wananchi haki zao,”  alisema Benson. Aliongeza kuwa katika utumbuaji majipu unaofanyika, umekuwa kwa asilimia kubwa ukilenga majipu madogo (viongozi wa chini) na kuacha viongozi wakubwa mafisadi bila kuchukuliwa hatua yoyote. Benson alitoa mfano wa ubakwaji wa demokrasia akisema ni kitendo cha Serikali kuingilia mihimili mingine, Bunge na Mahakama, ambapo kwa Bunge Serikali ina da...