Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda
Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘masoko’ yao mitaani limeshindikana baada ya hivi karibuni kuonekana kwenye vijiwe vyao, Ijumaa linakupa zaidi. Usiku wa Jumatatu na Jumanne iliyopita, makamanda wa kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kiliingia mitaani usiku wa saa nne kwa lengo la kuona kama madadapoa hao wamerudi baada ya kuadimika hapo kati kufuatia agizo la Makonda. OFM ilifanikiwa kuzunguka kwenye vijiwe vya Sinza- Afrika Sana, Sinza Mori (barabara ya kuelekea Meeda Bar), maeneo ya Corner Bar, Kinondoni, Buguruni na Manzese Tip Top jijini Dar na kufanikiwa kuzungumza na baadhi yao licha ya kuwa wakali. “Tumeamua kurudi kwa sababu ya njaa. Serikali iliposema tutoke mitaani ilitakiwa kutupeleka sehemu kufanya kazi au kutupa mitaji ya kufanyia biashara. “Kitendo ch...