Richard BBA: Canada Hali Mbaya
Mshindi wa BBA mwaka 2007, Richard Bezuidenhout Imelda Mtema Mara nyingi kumekuwa na sintofahamu kwa washindi wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) kwa hapa nchini mara tu baada ya kukabidhiwa kitita chao. Wengi wa mashabiki wa shindano hilo wanakuwa na shauku ya kuona maendeleo ya washindi hao kupitia fedha walizopata. Richard Bezuidenhout ni mshindi wa BBA mwaka 2007, ambaye kwa sasa maisha yake anayafanyia nchini Canada, akiwa na mkewe na watoto wake wawili huku akijiendeleza kimasomo. Mshindi huyo alifanya mahojiano na gazeti hili moja kwa moja kutoka nchini Canada. Kwa nini alipotea? “Sijapotea ila nipo nchini Canada na ndiyo makazi yangu kwa sasa kwa kuwa najaribu kuwapatia vijana wangu maisha bora kama vile elimu na huduma nzuri za afya.” Nini kilimfanya kuhamia Canada? “Kikubwa zaidi ilikuwa ni shule kwa kuwa nilikuwa nasoma chuo kimoja kinaitwa NATI (Northern Albert Instute of Technology) na baada ya kumaliza masomo yangu nimeanza kutengeneza filam...