Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kichwa Cha Binadamu Kuanza Kupandikizwa kwa Operation Kwenye Mwili wa Mtu Mwingine

Kichwa Cha Binadamu Kuanza Kupandikizwa kwa Operation Kwenye Mwili wa Mtu Mwingine

Picha
Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine, ifikapo mwakani.  Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant) Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya mwili.  Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya kutibu waliopooza mwili.  “Ningesema tuna takwimu nyingi zinaendelea, ni muhimu kwa watu kuacha kufikiria jambo hili sio rahisi, hi...