Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mapokezi Ya Rais Wa Sudan Salva Kiir Ikulu Jijini Dar Es Salaam Na Utiaji Wa Saini Kujiunga Na Jumuiya Ya Afrika Mashariki

Mapokezi Ya Rais Wa Sudan Salva Kiir Ikulu Jijini Dar Es Salaam Na Utiaji Wa Saini Kujiunga Na Jumuiya Ya Afrika Mashariki

Picha
Rais wa Sudan Kusini Mhe. Jenerali Salva Kiir leo ametia saini mkataba wa nchi yake kujiunga rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Kiir ametia saini mkataba huo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.  Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na Jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda kabla ya Rwanda na Burundi kujiunga na jumuiya hiyo baadaye.  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa  wakimsubiri  Rais wa Jamhuri ya Su...