Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Spika Job Ndgai Awagomea Wabunge Waliotaka Utaratibu wa Kusaini Mara Mbili Kwa Vidole Ufutwe

Spika Job Ndgai Awagomea Wabunge Waliotaka Utaratibu wa Kusaini Mara Mbili Kwa Vidole Ufutwe

Picha
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amejibu mwongozo ulioibuliwa na wabunge bungeni wa kutaka utaratibu wa kusaini kwa kutumia kidole mara mbili kwa siku uondolewe, kwa kusisitiza kuwa utaratibu huo hautabadilishwa. Majibu ya mwongozo huo aliyatoa bungeni Dodoma jana wakati akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago (Chadema), aliyemtaka Spika autolee majibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Konde Khatib Said Haji hivi karibuni wa kutaka utaratibu huo ufutwe. “Mheshimiwa Spika inaonesha kuna dalili ya Bunge lako kutojibu miongozo inayoulizwa hapa bungeni. Hivi karibuni tuliuliza juu ya namna ya kusaini kwa kutumia madole sijui kidole lakini mpaka leo hatujapatiwa majibu,”  alisema. Akijibu mwongozo huo, Ndugai alijibu kwa kifupi kuwa utaratibu wa kusaini wabunge ni mara mbili kwa siku na wanatakiwa wakandamize kidole chao hadi taa ya kijani iwake ndipo watakuwa wamesajiliwa rasmi. “Nataka nitoe ufafanuzi, nasikia kuna malalamiko juu ya utaratibu wa ...