Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Live Tena!
LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine ametengeneza habari, amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Risasi Jumamosi limepewa mchapo. PICHA ZADHIHIRISHA Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika mapozi ya kimahaba huku wamevaa mavazi ya kulalia (angalia picha Uk. 1). Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake. TUJIUNGE NA CHANZO Chanzo makini kilicho karibu na Dimpoz, kimepenyeza habari kuwa, licha ya Wema kupitia uhusiano tofauti, Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui. “Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si m...