Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kikwete: Nchi za Afrika Haziwezi Kukwepa Misaada ya Wazungu

Kikwete: Nchi za Afrika Haziwezi Kukwepa Misaada ya Wazungu

Picha
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika haziwezi kukwepa misaada kutoka nchi za Ulaya kwa kuwa misaada hiyo ni jukumu lao la kihistoria. Kikwete alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayohusu ‘Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2030’. Mkutano huo umejikita kujadili lengo namba 16 linalohimiza haki, amani na jamii shirikishi, hasa katika masuala ya utawala wa sheria kama chachu ya maendeleo endelevu. Kikwete alisema jukumu hilo linapaswa kuendelezwa kwa kuwa maendeleo ya nchi za Ulaya yalitokana na rasilimali walizozitoa Afrika kipindi cha ukoloni. Alisema nchi za Afrika zina rasilimali za kutosha hivyo, ili zifanye kazi bado kunahitajika uwekezaji ambao utaweza kuinua viwanda na kukuza uchumi wa nchi za Afrika, kwani bila hivyo itachukua muda mrefu kufika mbali kiuchumi. Hata hivyo, alisema nchi za Afrika lazima zijiwekee utaratibu wa namna ya kupokea misaada hiyo, lakini l...