Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa

Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa, Aagiza wasilipwe Posho wakisusa

Picha
Hatimaye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson ametoa maamuzi kuhusu hoja ya wabunge kulipwa posho au kutolipwa wanapoingia Bungeni na baadae kutoka nje kwa shughuli zisizo za Kibunge. Akisoma muongozo wake muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jioni hii baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, Dk. Tulia alisema kuwa wabunge wanaofanya vitendo hivyo hawatalipwa posho. Alitoa uamuzi huo baada ya kurejea kanuni za Bunge akitumia kanuni ya tano fasili ya kwanza ya toleo la mwaka 2006 na maamuzi yaliyowahi kufanywa na Spika waliotangulia katika hali kama hiyo. “Hivyo basi, kwakuwa jambo hili halikubaliki, na kwakuwa miongozo kadhaa imeshatolewa kuwasihi waheshimiwa Wabunge wasitoke nje ya ukumbi wa Bunge kwa shughuli zisizo rasmi.  "Naagiza kwamba wabunge wote wanaojisajili kisha kutoka ukumbini kwa kususia vikao vya Bunge, hawatastahili kulipwa Posho kwa si...