Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kampuni ya Lugumi Yajitokeza na Kusema Mkurugenzi wake Hajatoroka nchi.....Bofya Hapa Kuisoma Taarifa Yao

Kampuni ya Lugumi Yajitokeza na Kusema Mkurugenzi wake Hajatoroka nchi.....Bofya Hapa Kuisoma Taarifa Yao

Picha
Lugumi  Enterprises ni kampuni iliyoandikishwa na kufanya kazi hapa Tanzania na imekuwa ikifanya kazi mbalimbali ikiwemo ununuzi na ufungaji mashine za utambuzi wa alama za vidole yaani Automated FingerPrint Information System (AFIS) Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS.  Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi. Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Kwa mujibu wa kumbukumbu za kampuni yetu, ukweli ni kwamba mkataba huu umetekelezwa nasi kwa ku...