Tumia unga wa dengu kung’arisha sura yako
Ni ukweli usiopingika kuwa kila mmoja anahitaji kuonekana mrembo au mwenye mvuto mbele ya watu wengine. Ukweli huu huwafanya wengi kuhangaika kutafuta urembo na vipodozi vitakavyowapendezesha. Tatizo linakuja ni aina gani ya vipodozi wanavyopaka watu, kwani wengi hukimbilia vipodozi vyenye kemikali vinavyosababisha kupotea kwa rangi asilia hata ugojwa wa saratani ya ngozi, ambayo mwisho wake husababisha kifo. Wengi bado hawajapata uelewa kuwa urembo wa asili unaweza kutumiwa na watu wa rika zote kwa kuwa haudhuru ngozi na kutokusababisha magojwa ya ngozi. Wapo wanawake wanaotumia vipodozi vya asili na ukiwaona sura zao huwa ni nzuri wakati wote na wanakuwa hawabadili uasili wa ngozi yao. Kama ni mweupe utakuwa ni mweupe vilevile ila atakuwa anaufanya uwe na thamani kwani wakati wote atakuwa aking’ara na kupendeza. Kama mweusi atabaki na rangi yake hiyo hiyo bali atakuwa ni mweusi wa kupendeza na kila wakati atatamanisha kwa sababu ya rangi yake ya asili. Leo tutaangalia nam...