Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Zitto Kabwe Awachokonoa Wabunge Wenzake..Ataka Posho zao Zikatwe Kodi

Zitto Kabwe Awachokonoa Wabunge Wenzake..Ataka Posho zao Zikatwe Kodi

Picha
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewachokoza tena wabunge baada ya kuitaka Serikali kuanza kukata kodi katika posho za wawakilishi hao ili kuongeza wigo wa mapato. Zitto amesema hatua ya Serikali kuondoa msamaha wa kodi katika malipo ya kiinua mgongo cha wabunge katika bajeti ya Serikali ya 2016/17 ni jambo jema lakini isiishie hapo kwa kuwa viongozi hao bado wana mapato mengi yasiyokatwa kodi yakiwemo ya posho. Kauli ya mbunge huyo wa Kigoma Mjini ni mwendelezo wa msimamo wake wa kupinga wabunge kulipwa posho ya vikao bungeni na katika Bunge la 10 alipokuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) aliongoza kampeni ya kupinga ongezeko la posho hiyo bila mafanikio. Aidha, pendekezo lake kutaka posho za wabunge zikatwe kodi limekuja siku mbili tangu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson atangaze kukata posho za wabunge watakaokuwa wakisaini kuingia bungeni na baadaye kuondoka na waathirika wa kwanza wa hatua hiyo watakuwa wapinzani wanaosusia vikao vyake. Akitoa maoni katika m...