RAIS WA ZAMANIBWA NIGERIA OBASANJO AIONYA UGANDA
Kampala. Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ameitaka Serikali ya Uganda kufanya mazungumzo na upinzani ili kuondoa uhasama uliojitokeza baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu siku chache zilizopita Obasanjo ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya Madola uliokuwa ukiangalia vigezo vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda wiki iliyopita, amewashauri viongozi waUganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao. Obasanjo alikemea jinsi Serikali inavyotumia nguvu kuwadhibiti wapinzani na kutaka uhuru wa kujieleza uheshimiwe. ‘’Dosari zilizotokea katika Uchaguzi Mkuu zimeathiri matokeo na kutilia shaka ukweli, haki na uwazi wa uchaguzi huo,’’ alisema kiongozi huyo wa zamani wa Nigeria. Pia, alisisitiza tofauti kati ya Serikali na upinzani zinahitajika kusuluhiswa kupitia mazugumzo na siyo vinginevyo. ‘’Vyombo vya usalama vinatakiwa kuacha tabia ya kukamata viongozi wa siasa na badala yake walinde usalama kwani wanasababisha...