Navy Kenzo ni mfano wa kuigwa kwa wasanii waliokata tamaa kwenye muziki
Navy Kenzo ni kundi linaloundwa na wasanii wawili, Aika na Nahreel. Hakuna asiyejua kuwa Aika na Nahreel ni wapenzi kwa muda mrefu kabla hawajaingia kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva. Mwanzo kabla ya kutengeneza kundi la Navy Kenzo walikuwa kwenye kundi la Pah One ambalo walifanikiwa kuachia nyimbo kadhaa kama, ‘Ghetto’ na ‘I Wanna Get Paid’. Aika na Nahreel walifanikiwa kuachia nyimbo kadhaa wakati wanaanza ndani ya Navy Kenzo ambazo hazikufanikiwa kufanya vizuri na kupenya kwenye ngoma za masikio ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva. Nawapongeza kwa uvumilivu wa muda mrefu, na sasa wanaanza kuona faida ya muziki wao. ‘Game’ ni nyimbo ambayo hawataisahau kwa maisha yao yote. Ujasiri wao wa kuwekeza hela nyingi kwenye video ya wimbo huo na kufanikiwa kufanya video nzuri chini ya Justin Campos ulivifanya vituo mbalimbali vya TV barani Afrika vicheze wimbo huo. Mwaka mmoja kabla walionekana ni kama wasanii wa...