Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya AJIMILIKISHA SHAMBA LAHEKARI 4000

PROFESA ANNA TIBAIJUKA KITANZINI TENA,AJIMILIKISHA SHAMBA LAHEKARI 4000

Picha
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk Charles Mlingwa wamelipuliwa bungeni wakidaiwa  kutumia madaraka yao vibaya. Tuhuma hizo zilitolewa jana na wabunge wa upinzani Conchesta Rwamlaza (Viti Maalum - Chadema) na Dk Godwin Mollel (Siha - Chadema) walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Rwamlaza alidai kuwa katika Kijiji cha Kamwila wilayani Muleba, Profesa Tibaijuka akiwa serikalini, aliomba eka 1,098 lakini hivi sasa anamiliki eka 4,000 jambo ambalo linazua mgogoro na wananchi. “Hili linaleta matatizo kwa kuwa haiwezekani mtu awe na eneo hilo lote halafu anakodisha kwa wananchi,” alisema Rwamlaza. Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo na kama Profesa Tibaijuka aliomba heka 1,098 apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizonazo hivi sasa. Dk Mollel alimtaka Waziri Mkuu amhamishe Dk Mlingwa akidai ni tatizo katika wilaya hiyo. Alisea juzi ulitokea mgogoro kati ya wananc...